Tuesday, July 31, 2012

WANA HABARI KAMA HAMJUI SHERIA KAENI KIMYA.

VYOMBO VYA HABARI NI KERO MGOMO WA WALIMU

Kila mtu na weledi wake. Taaluma ni kitu cha msingi sana. Kila mtu ni mjuzi katika fani aliyoisomea. Na leo hii ndio maana kuna mgawanyo wa kazi. Sio kila mtu afanye kazi zote.

Mwalimu akafundishe, mwana habari akatupashe habari, wanasiasa wakatudanganye, nakadhalika, nakadhalika.

Sote tunajua ambavyo walimu wamekuwa katika mgogoro wa kimaslahi na serikali uliowapelekea kugoma hivi juzi. Walimu hawa watakuwa halari kugoma iwapo wametimiza matakwa ya mgomo harali kama yalivyoainishwa katika sheria ya kazi na mahusiano kazini ya mwaka 2004, no 6 katika kifungu cha 80(1) (a)-(e).

Sheria hii pia katika kifungu cha 86(7)(a) kinataja wazi uhuru wa wafanyakazi kugoma iwapo CMA wameshindwa kutatua mgogoro wao wa kimaslahi.

Katika sheria hii hamna sehemu ilikoruhusiwa mgogoro wa kimaslahi kuupeleka mahakamani au kwa mtatuzi yaani Arbitrator. Kitendo cha Serikali kuamua kuupeleka mgomo wa wlimu mahakamani ni udhaifu na ni kudhiirisha kushindwa kwa serikali na kutapatapa.

Sasa kinachonitia wazimu hadi kichefuchefu ni hawa waandishi wa habari wasiojua chochote kuhusu migogoro na sheria mahala pa kazi kujitia kimbelembele kukosoa juhudi za walimu kudai haki zao.

Waandishi wa habari na watangazaji sijui kama wanaijua vema sheria ya kazi! Utasikia wakisema walimu wamo katika mgomo usio halari! Nani kasema si halari? Je, uhalari wa mgomo unategemea sheria au jinsi wewe unavyowaza!

Hacheni ushabiki na ukibaraka wa mambo msiyoyajua. Mahakama pekee ndiyo itasema iwapo mgomo ulikuwa harali au la lakini sio wewe uliyelala ukaamuka na mawazo yako ukatutangazia.

Kufanya kazi katika mazingira magumu, ujira mdogo, sheria ngumu za kazi na ubabe katika mazingira ya kazi havina budi kupingwa kwa nguvu zote n a kila mtanzania mwenye kutaka maendeleo.

Heko walimu, umoja, nguvu, pamoja.

Sunday, July 29, 2012

KATIKA HILI MANAGEMENT TAASISI YA USTAWI WA JAMII HAMKUFIKIRIA

ADA TAASISI YA USTAWI WA JAMII NI KUZUNGUMKUTI CHA FADHILI

Nilipopewa prospectus kwa mara ya kwanza kabisa hivi majuzi, haraka nikazikimbilia kurasa zenye kuonesha mpangilio wa ada kwa mwaka huu. Nilishutuka sana. Niliona kuwa mfumuko wa bei sasa umeingilia hata ada.

Nilisikitika kuona kwamba management kwa kusaidiana na bodi ya ukurugenzi wameamua kupandisha michango chuoni hapo kwa takribani asilimia elfu moja (1000%).

Gharama ya usajiri imepanda toka Tsh 5000/- adi Tsh 50,000/-, fomu za maombi ya kujiunga zimepanda kutoka Tsh 30,000/- adi Tsh 50,000/-, kitambulisho kimepanda toka Tsh 5000/- adi Tsh 15,000/-, ada ya hostel sasa ni shilingi 400,000 kutoka 250,000 ya zamani.

Ni vi tuko. Kwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu ngazi ya shaada ya kwanza atarazimika kulipa shilingi milioni mbili na nusu (2,500,000) kama ada ya mwaka kutoka milioni moja na elfu mbili (1,002,000) malipo ya zamani.

Mbaya zaidi ni kwa mwanafunzi anayeomba kuhairisha mtiani kwa sababu zinazoweza kumzuia kufanya mtihani kwa utulivu huyu atarazimika kulipa shilingi laki moja (100,000) kwa ajiri ya kukubaliwa ombi lake.
Mtihani wa mwisho wa semester tangu sasa utakuwa ukilipiwa shilingi elfu sabini (70000).

Hapo ndipo nilipoona Taasisi imechoka. Wapo watu wanaoshindwa kulipa ada ya semester na hivyo kutoruhusiwa kufanya mtihani, leo hii mnasema hata mtihani tunaulipia! Haya ndio maajabu ya Taasisi.

Katika mfumo wa vyuo vikuu tanzania, na taasisi za elimu ya juu nchini, ni Taasisi ya Ustawi wa Jamii  pekee inayotoza ada kubwa kwa mwaka kwa mpango wa sasa.

Chuo hiki ambacho bodi ya mikopo wamekiondolea udhamini wa mkopo sasa mnataka mtu alete miliono mbili na nusu! Aitoe wapi? Hiki ni chuo cha serikali chenye udhamini wa serikali kwa asilimia kadhaa sasa mbona mnatutupia zigo zito lililojaa misumari inayochoma!

Sasa mwanafunzi atalazimika kukilipa chuo shilingi laki mbili (200,000) kama ela ya Field Work Practice na shilingi laki nne (400,000) kama ela ya research!

 Hivi bodi ni watu au mashine? Wanafahamu uchungu na ugumu wa maisha? Mbona wanatutesa hivi? Kama bodi haipo kwa maslahi ya wanafunzi na mstakabali wao basi haitufai!

Leo parking ni shlingi 2000. Si kwamba nalalamika kwasababu nina gari. La! Asha! Hii ni pesa nyingi. Tangu lini mtu akalipia parking ya nyumbani au eneo ulikoenda kununua huduma.

Nijukumu la Taasisi kutafutia wateja wake parking na sio kuwatoza pesa zote hizo.

Mimi nashauri michango isiyokuwa na msingi iondolewe ili kuwapa wanafunzi hauweni. Uhai wa Taasisi u mikononi mwetu na kwa namna hii taasisi tutaizika.

NIDA WAMEKURUPUKA KATIKA ZOEZI LA VITAMBULISHO VYA TAIFA

KATIKA ZOEZI ZIMA LA VITAMBULISHO VYA UTAIFA, NIDA MMEKURUPUKA.


Ni hivi karibuni ambapo taifa letu limeingia katika mchakato wa kutoa vitambulisho vya utaifa kwa wakazi wote nchini na watanzania wote.

Zoezi hili linasimamiwa na taifa chini ya wakala wa vitambulisho vya taifa NIDA. Kusema kweli NIDA wamekurupuka katika kuanzisha utekelezaji wa mpango huu wakianza na mkoa wa Dar es salaam. Pamoja na yakuwa siku walizotoa hapo hawali kutotosha bado NIDA hawakufanya tathmini ya hawali kujua idadi ya wakazi katika vitongoji vya mkoa huu.

Zipo sehemu zenye wakazi wengi kupindukia na bado wameweka kituo kimoja cha kuandikia watu katika kata moja. Hili limezua fujo katika vituo hivyo watu wakigombea kuandikwa. Wakazi wa jiji la Dar es salaamu kwa siku kadhaa sasa wameailisha shughuli zao za msingi wakishinda katika mistari wakingoja kuandikwa.

Aidha, mbali na kuwa vituo vya uandikishaji kufunguliwa asubuhi ya saa mbili, watu wamekuwa wakifurika vituoni hapo tangu saa kumi usiku kuwai kile wanachokiita namba.

Pamoja na adha hii, bado kumekuwa na utaratibu mbovu unaoshindwa kuwabaini watu waliowai. Hali hii imesababisha watu kutumia nguvu zaidi katika zoezi hili badala ya utaratibu na utu.

Zoezi hili limeonekana pia kuvutia rushwa kwa watendaji na kutoa huduma kulingana na mtu anavyojulikana.

Ni ombi langu sasa NIDA watakapokuwa wameamishia zoezi hili mikoani wajitaidi kuboresha huduma zao ikiwa ni pamoja na kuweka ulinzi vituoni kulinda usalama wa raia. Pia NIDA wajaribu kufikiria uwezekano wa kuandikishwa na kupiga picha kwa wakati mmoja. Mbali na kwamba zoezi hilo litaokoa muda bado gharama za uendeshaji na usumbufu vitapungua.

Niseme, vitambulisho vya utaifa ni suala la maana sana. Ni vyema kila raia kujiandikisha kupata utambulisho huu. Utaratibu ubooreshwe ili kutoa mwanya kwa watu wengi kujiandikisha. Vituo vya kujiandikisha viwekwe vingi kulingana na uwingi wa watu wa eneo.

Saturday, July 7, 2012

                          MCHAGUE FRANK JOHN KWA MAENDELEO YA ISWOSO.


Twendako sio mbali. Sio mbali hata kidogo. Ni punde tu!

Naliposema BIR II tushikamane nilimaanisha hili. Sasa yametimia.

Ndugu yetu, mwenzetu ndg Frank John anawania kinyang'anyiro katika harakati za kuitwa raisi wa iswoso. Akiwa na kauri mbiu yake naamini kijana amekuja kutatua matatizo ya walio wengi.

Kama nilivyowai kuandika katika mtandao huu, natumai kijana anajua ni kwanini anaitaji kuingia ISWOSO. Madhaifu na mapungufu yaliyooneshwa na serikali dhaifu inayomaliza muda wake hayafai tena kujirudia.

Frank ni mfananishe na sauti iliayo nyikani, itengenezeni njia yake, yanyosheni mapito yake, kila bonde na lijazwe, na mashimo yafukiwe ili kijana aingie Ikulu.

Ndugu zanguni, hatutamchagua Frank kwasababu yeye ni IR bali kwa uweza wake mkubwa wa kutenda shughuli mbalimbali.

Ni dhairi yakuwa kijana amekuwa akijituma sana katika kuakikisha gurudumu la maendeleo ya chuo chetu likienda mbele. Amekuwa wa kwanza katika kufuatilia mikopo huku akijitoa mhanga hata kulikosa  darasa kwa kufuatilia mambo yanayotuhusu sote.

Ni upendo wa hajabu huu ambao mtu anakuwa tayari kujitoa mwenyewe kwa ajiri ya watu walio wengi. Huyu ndiye yule anayetufaa.  Hiyo ndiyo nyota ya mashariki waliyoiona mama jusi nyakati za mfalme Helode.

Tuziweke kando tofauti zetu za course na kumchagua mtu afaaye. Hebu tuvunje mwiko. Tuamini inawezekana. Mabadiliko ni muhimu na yanaanza na sisi.

MCHAGUE FRANK JOHN KWA MAENDELEO YA CHUO CHETU

Friday, June 15, 2012

                                                TATIZO NI SISI NA SIO USISI




Salaamu sana ndugu zangu nikitambua fika yakuwa mnaendelea na kazi nzito ya kulijenga taifa letu hili changa la Tanzania. Mimi leo nawajia, nakuja na hili.

Tujikumbushe story ya zamani tuliyoisoma tukiwa drs la pili hivi. Story hii inamuhusu popo. Swali ni je, popo ni ndege ama mnyama. Mwisho wa kigano hiki ntakutaka kunijibu swali hili.

POPO NI NDEGE?

Hapo zamani za kale wanyama wote waliishi mstuni. Binadamu aliishi peke yake huko kwenye makazi yake mbali na hao wanyama. Kila mara binadamu alikwenda mstuni kuwinda wanyama na ndege kwa ajili ya kujipatia kitoweo. Tabia hii ya binadamu ya kuwaua ndege hovyo na wanyama iliwakasilisha sana wanyama hao wakazi wa mstuni.

Wanyama kwa pamoja waliazimia kukutana kuweka mikakati kwa ajiri ya kuikomesha tabia hatarishi ya binadamu. Ndege nao wala hawakubaki nyuma. Nao walianzisha vikao vilivyokuwa na maana moja ya kumsambaratisha binadamu.

Wanyama walianzisha vikao kwa nguvu zote. Wakawekeana maazimio na mikakati ya kuhakikisha mwanadamu hagusi tena himaya ya wanyama hao. Sungura alifuatia baada ya kongoni kumaliza maongezi yake. Sungura akaanza kwa kusema; "ndugu zanguni, najuwa nyote mnajua fika yakuwa ndugu zetu wengi wameishia mikononi mwa mwanadamu na kugeuzwa kitoweo." Sungura aligeuka kushoto kisha kulia. "Amini msiamini jukumu la kumshinda mwanadamu ni letu sote pasipo kumbagua mtu. Wakale walisema umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Kama hatutatafakari vyema ya wahenga tutaishia kuwa supu katika bakuli la mwanadamu. Mimi ninalo wazo," "mh!" wanyama wote waliitikia kisha sungura akaendelea; "Nadhani ndugu zanguni tukienda kuhemea huku na kule tusiende tofauti. Twende kwa umoja wetu. Tena yatupasa tutengeneze filimbi kila mmoja wetu awe nayo. Popote mwenzetu atakapomwona mwanadamu basi apulize  kipenga  nasi tutajua hatari inayotukabiri." Alimaliza sungura mazungumuzo yake na kuketi chini. 

Wanyama wote waliafikiana na wazo la sungura na kuazimia kumtafuta mtaalamu wa kutengeneza filimbi hizo. Wanyama wote walitawanyika na kuagana kila mtu akienda kuzitekeleza kazi za siku. Kuutafuta mkate wa kilasiku wa kwao pamoja na watoto wao.

Huku mkutano wa wanyama ukiendelea, ndege nao hawakubaki nyuma. Mkutano wao ulifanyika juu ya mbuyu. Ndege wote waliitikia mwito wa mwenyekiti wao mh. Mbuni. Lamgambo lilipolia, ndege wakazitanda mbawa zao juu ya hanga mbio kuelekea eneo la tukio.

Popo naye akajifunga kibwebwe kuelekea kunako mbuyu. Hakutaka hili la leo limpite. Haraka haraka akajichanganya na wenzie.

Mkutano ukaanza. Mwenyekiti alianza kwa kuwakaribisha ndege wote, popo naye yu miongoni mwao. Baadae akatoa fursa kwa ndege wengine kutoa mawazo katika mchakato wa kumkabiri adui yao.

Kanga alikuwa wa kwanza kuinuka. Baada ya kuzikunguta mbawa zake, kanga alianza kwa kusema; "ndugu zaangini mliopo mahali hapa. Natumai sote tunaguswa na tatizo hili zito. Mwanadamu ametufanya chakula kitamu kwake. Ama hakika, yatufaa tumshinde na siraha yetu kuu ni umoja. Tukiwa wamoja kila kitu kitawezekana. Mimi niseme yakuwa itakuwa vyema kama sote tutaungana na kuitetea haki yetu." alimaliza kanga. Sasa ilikuwa zamu ya popo kuongea. Pasipo kujua kuwa anachunguzwa akaanza kupayuka. Maneno yake hayakuwaingia ndege wengine. Ndege wakaanza kujiuliza maswali, huyu jamaa sio mwenzetu au? Mbona ana meno? Lakini mbona ana mabawa na anapaa! 

Baadae njiwa akona isiwe tabu. Akamuuliza swali. "Samahani, mbona wewe una meno? Yamkini wewe utakuwa mnyama! Hapa hutufai. Popo akajitetea sana lakini lo! Ndege walisha mwondolea imani, wakamfukuza.

Popo akaona isiwe tabu, maadamu yeye ni mnyama basi ataudhulia vikao vya wanyama. Siku ya kikao cha wanyama ikafika. Wanyama wakakusanyika chini ya mti wa mwembe. Wakiwa wanaendelea, popo naye akajichanganya. Wanyama wakataharuki. Iweje ndege audhulie vikao vyao! Wakamfukuza. Akajitetea sana. Akasema pamoja na kuwa ana mabawa lakini bado ni mnyama maana anyo meno kama wao na anazaa kiumbe kamili. Neno la mwisho alilimaliza na kofi kali kutoka kwa mzee simba aliyekuwa kagathabishwa na maneno ya popo. Popo aliona nyota tu. Akatimuka mbio kuelekea kwake na kwa aibu akaapa kutotembea mchana. Yeye akapanga mipango yake ataifanya usiku kufuta haibu iliyompata.

Adi leo popo ujificha mchana na kutoka usiku kutafuta chakula. Hii si kwasababu popo anapenda bali hali iliyomsibu.

Hadithi hii inanifundisha nini? Mtu naye anaweza kuwa kama popo. Asiwe mnyama wala ndege! Dunia hii kweli ni hatari. 

Kitu gani kinatufanya tupoteze mwelekeo na kutokuwa na upande kama popo? Watu tunakuwa kama bendera. Upepo ukipepea kuelekea kusini nawewe kusini, ukigeuzia mashariki nawewe mashariki. Sasa tofauti kati ya m2 wa namna hii na demu ambaye kwa muda umpenda huyu lakini akiona mwenye mali zaidi ugeuza maamuzi yake iko wapi?.

Ndugu zanguni, ndugu wa damu, BIRA II. Tatizo sio usisi, tatizo ni sisi. Wana BIRA II, mioyo ya unafiki hatuijui? Mbona tunaangaika kutakatisha kaniki wakati rangi yake tunaijua?  

Zimeanza kuwepo taarifa kuwa kitakacho tudondosha BIRA II katika mbio za urais ni moyo wa usisi uliojengeka miongoni mwa wanafunzi tulio wengi. Hili nalikataa kwa herufi kubwa. Sio kweli hata kidogo. Hii ilikuwa mikakati tuliyojiwekea kama darasa kuhakikisha tunashinda chaguzi zijazo. Haukuwa usisi bali uungaji mkono wagombea watakaojitokeza drsn kwetu. 

Tatizo limekuja kuwa ni unafiki, ushushushu wa kupeleka habari za ndani za darasa nje ya darasa kinyume ya utaratibu na makubaliano. Ujuaji unazidi kututafuna taratibu kama mchwa! Naikumbuka kauli moja aliyoitoa SAMWELI darasani kipindi fulani na namnukuu; "tatizo ni hilo. Umu ndani kunawatu wanaodhani kuwa kuna watu waliokuja kusoma na waliokuja kuongoza. Kwa upumbavu huu tutabakia kuwapigia kura wenzetu na kuwapigia makofi. ISOSWO tuzidi kuisikia tu. Na kama kulikuwa na wakati mzuri wa sisi kuingia madarakani ulikuwa ni mwaka huu." mwisho wa kumnukuu. 

Haya maneno hayajachuja. Katika unafiki wa namna hii, hatuwezi kamwe kuitawala isoswo. MWENYEZI MUNGU katika kitabu cha Ufunuo anasema dhairi yakuwa hataki watu wa uvuguvugu. Kama ukiamua kuwa wa moto basi kuwa wa moto kabisa na kama ukiamua kuwa wa baridi uwe wa baridi kwelikweli.

Ukweli ni hivi, hata mimi nawachukia watu wa uvuguvugu. Kama kweli we ni wa moto basi kuwa wa vile. 

Ndugu zanguni, usisi ni suala linalofaa kupigwa vita ila umoja wetu kama BIRA II ubaki palepale. Mimi nimesema hayo. Wadau ni ninyi. Ni bora kukaa kimya kuliko kujibu swali tusilolijua. Darasa ni sisi na sisi ni darasa. Uhai wa darasa uko mikononi mwetu. Tuubinye ufe au tuuachie uruke. TATIZO SIO USISI, TATIZO NI SISI.

By Jonas John R.

Saturday, June 2, 2012

                                                     SIKU HILE IJAYO


Sijui ninini Mungu alimaanisha lakini ukweli ndio huo ya kuwa kwake siku elfu moja ni sawa na siku moja. Kama hivyo ndivyo ilivyo, basi hakuna mtu duniani ambaye aliwai kuishi duniani zaidi ya siku moja. Katika nyakati hizi ambamo shida za dunia zinaweza kumfanya mtu atamani kuukatisha uzima, bado Mungu anaona umeishi nusu siku.

Hachana na hayo. Kwa mwanadamu mambo ni tofauti. Siku njema uisha mapema kabisa na kukuachia maumivu ya kuikumbuka siku hiyo. Mfano; siku ambayo umekutana na marafiki zako wa kitambo. Mnacheka mnapiga soga. Mambo si ndo hayo. Siku hii ingekuwa vyema kama ingerefuka kidogo kuutoa mwanya kwa ndugu hawa kuongea zaidi. Lakini hakuna.

Kadhalika siku mbaya kwa ubaya wake yaweza ikagoma kuisha. Siku moja ikawa kama miaka mia. Jitihada zako za kuitaka siku ikatike mapema zikagonga mwamba. Hilo ndilo jambo baya zaidi japo sina maana ya kuwa kwa Mungu siku zote ni mbaya.

Kadhalika mwaka mmoja waweza kuuona kama miaka elfu ikiwa siku hazijakwendea vyema. Ndiyo, makosa madogo ambayo unaweza kuyafanya mwanzoni mwa mwaka yaweza kufanya mwaka huo uwe mrefu kweli kweli.

Fikiri muhula wa kuchagua viongozi. Kama mtafanya utani na kujipatia viongozi mabuda mwaka huo hakika utakuwa mrefu kwenu maana viongozi watawatia kinyaa.

Sasa hili tunalijua. Huu ni wa kati wa kusema inatosha. Katika jamii yetu ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii tunayo nafasi sasa ya kubadilika. Tusikariri. Kosa tulilolifanya miaka michache iliyopita kujipatia viongozi hewa limetughalimu sana. Sasa ni wakati wa kuangalia utendaji zaidi kuliko mishabiko isiyokuwa na maana yoyote.

Kiongozi bora mwaka huu ni razima ajikane mwenyewe ajitwishe msalaba wake alafu aingie ikulu. Nina maana gani? Kama kuna mtu anataka kuwa kiongozi kwa kusukumwa na watu pasipoyeye kuona ninini anaitaji kuingia madarakani atufanyie, basi hatufai.

Mtu anayegombea ni vyema akawa anatambua ni wapi uongozi huu umevurunda na yeye anataka kuparekebisha. Kama haoni chochote huyo naye ni bomu! Hapana mtu kuingia kwa kisingizio cha kupendekezwa. Huyu akiharibu ataanza kusema kuwa yeye hakuwa tayari kugombea isipokuwa kwa matakwa ya wengine.

Hatumchagi mtu kwa usocial work wake au u-IR wake. Tunayemtaka ni kiongizi wa iswoso. Maana hiyo dhambi ya ubaguzi tutaipeleka wapi. Kwamba japo anaweza lakini tatizo ni IR au social work! Nasema likija hili tena, hatutaliepuka hili la uongozi tulionao. Ni haibu, fedheha na na.. sijui na nini!

Mtu akajiweke katika mizani ajipime mwenyewe. Kugombea sio fashion. Kama huwezi achia wengine. Na kipimo ndo hiki; unajua ni wapi uongozi huu ulikokosea? Je, unayajua matatizo ya chuo chetu? Unajua yakuwa mpaka sasa kuna mfumo tunaoutumia unaokifananisha chuo hiki na chuo cha kata? Kama katika haya unaona maluweluwe hacha kabisa maana hujifai mwenyewe na hutufai sisi.
Jonas R.

Sunday, May 27, 2012

MAVAZI NA UTAMADUNI WA MWAFRIKA


Nimerejea tena uwanjani. Ni katika kudadisi na kudadavua hili na lile. Leo ninalo suala moja tu nalo ni hili, "Lipi vazi linatufaa kama vazi la taifa".

Ninaposikia yakuwa kuna mpango wa watanzania kuletewa vazi la taifa ninapata shaka kiduchu! Hivi watanzania wa leo ususan vijana wanaotamani kutembea uchi wa mnyama barabarani watakubali kuvaa vazi hilo la taifa?

Kila nikijaribu kuwaza sana majibubu yanazidi kuwa mbali zaidi. Hivi utamaduni wa mwafrika tumeutupa wapi? Suala gani limezifanya mila zetu za zamani kufukiwa shimoni na kuiga yale ya wageni! Sisi mbona tunatia huruma jamani. Tunaukataa usisi na kuutukuza uwale! Huu ni upuuzi usiokuwa na msingi wowote.

Dada zetu nani amewaloga. Au msemo nyinyi ni maua nanyi mmesadiki. Kitu gani kinawafanya mtembee barabarani mkiwa uchi? Mbona mmesahau haya, au hamjui yakuwa nyinyi ni wazuri. Yaani mnapendeza hata msipojiremba. Sasa nyinyi badala ya kujilemba mnatembea uchi! Lo!

Mimi niseme hakuna mwanadamu aliyeumbwa na maungo ya kuvutia kama mwafrika (binti). Sasa kitu gani kiwafanye mjiuze miili yenu sokoni kama dagaa wa Kigoma wakati nyinyi ni lulu? Na hayo maziwa yenu mbona mnayafunga Tanganyika jeki nyinyi mnasema eti mna boost kidogo! Huu ni upuuzi kabisa. Wengine mnatumia dawa kuongeza ujazo wa maziwa yenu! Mmelogwa?

Yaani maziwa yakituna tena yakawa nje ndo mnapendeza? Hapo mmedanganywa mkadanganyika. Tena mnazo nguo mnaziita bluetooth. Yaani hizo mkivaa tunaona ama chup au tight. Iz it fair? Binti kupanda daladala watu uwape shida, ya nini?

Sasa kuna mtindo mpya. Eti mnasema taiti ndefu. Mwana dada kakupigia hiyo taiti ndefu na ki-topu. Ehh! Barabarani utadhani mwenda wazimu anapita!

Nanyinyi kaka zangu huu mtindo mmejifunza wapi? Hii nyinyi mnaiita kata kei. Sasa ndo kusema suruali haziwatoshi tena au ndo kutaka kurahisisha mambo? Mwanamume unamvutia nani na wewe? Umevaa nguo ya nje lakini chupi, boxer viko nje! Yaani kijana akiinama aibu. Sasa kama binti anafanya hivyo kutafuta soko wewe mwanamume unatafuta nini? Mimi nnavyo jua dume ndilo malanyingi linatongoza baada ya kuvutiwa! Sasa wewe na harakati za kutembea uchi mwanamume ni nini?


Ndugu zanguni tubadilike. Tusiyatupe maadili kwa kuiga mambo ya kigeni. Sawa hata mkitaka kujifunza baadhi angalia ni nini! Mbona hata mazuzu huchagua waokote nini jaani na sio kila kitu? Tubadilike; mabadiliko yanaanza na wewe. Fanya hivyo.
Jonas John R.
ISW

Monday, May 21, 2012

Apply leo kujihakikishia mkopo wako kutoka bobi ya mikopo Apply now through  heslb.go.tz then OLAS: welcome select your year under year1-year3. APPLY NOW.
                                          UMOJA NA MGAWANYIKO BIRA II-2012


Asalam aleykum wa ndugu zangu. Leo naja mezani tena kuuleta mjadala huu ambao umekuwa ukigonga vichwa vya wanafunzi kila kunapoitwa leo. Swali ni kwanini watu ndani ya BIRA II 2012 katika chuo chuo cha Ustawi Wa Jamii tuna mgawanyiko? 


Jibu la swali hili haliitaji kuwaza sana. Kwa mtu mwenye upeo na uwezo wa kupambanua mambo atajua tatizo liko wapi hata kwa kuangalia mwenendo ndani ya darasa.

Nivyema kujua ya kuwa palipo na watu sitini kuna tabia sitini. Kisaikolojia watu hawafanani kuwaza, kunia na kuamua. Katika watu watu wote hao wapo wenye tabia nzuri na mbovu. Wapo wenye polojo wengine mnasema eti majungu, wambea, wapole na hata wale wengine!

Ni vigumu kujaribu kuunganisha watu wote hawa wakawa kitu kimoja. Jitihada zote utakazozifanya ni sawa na kujaribu kumvisha sketi mbuzi. Mbali na kuwa hana kiuno cha kuvaa sketi bado hata yeye haipendi sketi maana inamkera.

Darasa hili lina umoja ila lina watu wenye mtazamo tofauti. Hakika mtu hasiyependa majungu yaani polojo hawezi kamwe kuchangamana na kinara wa polojo. Japo wale wakali wa polojo wako tayari kuchangamana na yeyote katika kutafuta wapi atachota majungu.

Yaipovunjika makundi yetu ya hawali na kuundwa mapya yasiyokuwa rasimi eti ya kujadili ndipo mambo yalipoharibika. Watu tukayasaliti makundi yetu na kuunda makundi mapya tukikaribishana ki rafiki, kitabia na kimengine. Pale drsa zima lilipokuwa na makundi yasiyo zidi manne ndipo baraaa lilipoanza. Ikawa sio mijadala ya masomo bali kumjadili huyu na yule. Tabia hii ililifanya darasa kuwa na mgawanyiko mkubwa kati ya makundi yasipenda majungu na yale yanayotanguliza majungu kwenye kundi kama sala ya kufunguli majadiliano (discusion)

Kiukweli wale wasiopenda polojo ni wamoja pale drsani na wale wapenda polojo ni wamoja pale darasani. Sio swala la kushangaa kusikia mtu akisema mimi siwezi kwenda kudiskasi na watu fulani maana wao ni watu wa majungu! Sasa hapa kuna la kuangaika kumtafuta mchawi wa darasa? Wachawi ni sisi wenyewe. Amini ya kuwa mtu wa polojo anaweza kuugua asipopiga umbea siku nzima. Sasa itakuwa shughuli haya makundi kukaa pamoja kuutafuta mwafaka isipokuwa tu mchezo wa ushushushu ukome.

Binafsi sipendi majungu hata kidogo. Kwa maana hiyo sipendi hata kuchangamana na wao. Ila tufaamu ya kuwa polojo nyingine ni nzuri zile zinazodumisha urafiki na hutani lakini sio majungu. Katika suala la tabaka mbili kuu yaani wapenda majungu na wasiopenda ni vigumu darasa kuwa na umoja.

Muda mwingine huwa nawaza pasipo kuwa na majibu. Hivi labda mtu anaponyanyuka na kuanza kuponda wengine kuwa wana majungu hivi ajiwazia kwanza yeye na kujiweka katika hatua hipi? Wawezaje kuliona banzi katika jicho la mwenzio na ungali hujaliono boliti katika jicho lako? Hebu fikiri eti mtu anayesifika kwa polojo asimame na kupinga polojo! Badala ya watu kumsikiliza wataanza kunong'ona wakijiuliza iweje kinara wa polojo leo aseme tena polojo haifai? Ki ukweli badala ya kuwafikishia watu ujumbe utakuwa umeharibu kabisa. Hau ndio kusema shetani akizeeka ujigeuza Malaika?

Tuache hizo. Hapana mganga atakayekuja kutibu hili, dawa tunayo. Tuache polojo zisizokuwa za msingi

Sunday, May 20, 2012


BODI YA MIKOPO NA USAJIRI MPYA!!!!!

Hule mfumo wa kujisajiri katika bodi ya mikopo kwa wanafunzi walioko vyuoni unendelea. Hakikisha unajisajiri sasa kupitia OLAS heslb. Ni muhimu kwako mwanafunzi uliyeko chuoni ususan mwaka wa tatu na wa nne. Do not miss. For more info fungua wavuti ya bodi ya mikopo

Thursday, May 17, 2012

                                                       TANZANIA NA RPM
Tanzania ni moja wapo ya nchi zinazoendelea. Hapana shaka ya kwamba katika kufikia miamoja utaanza na moja. Tangu tujipatie uhuru mwaka 1961, Tanzania imekuwa ikifanya jitihada za makusudi kuhakikisha maendeleo yanafikiwa kwa kutumia rasilimali zetu tulizo nazo.


Naamini kwa kiwango tulichofikia kinaelekea kutia moyo hususan kwa mwananchi anayeitakia maendeleo nchi hii. Kwa muda wa takriban miaka 50 ya uhuru, Tanzania imejitutumua na kujaribu kushughulika kwa sana kuwaletea wananchi maendeleo.

Tanzania ya sasa imejenga barabara nzuri za kusifika. Maeneo mengi ya nchi yetu sasa yanafikika ki urahisi kwa sababu ya ubora wa miundo mbinu tuliyonayo ususan barabara. Leo ni rahisi kwa mtu kusafiri kutoka Dar es salaam hadi kigoma kwa siku mbili tu mwendo wa basi. Tofauti na zamani ambapo ilikuwa ikimrazimu mtu kusafiri kwa takribani siku nne hadi tano kuitafuta Kigoma.

Dar es salaam hadi Mbeya kwetu wanasema 'kachwant'apasi'. Ninamaana gani? Leo waweza kutoka Dar kwenda kunywa chai Mbeya na kurudi Dar ukaendelea na zako shughuli. Vivyo hivyo hata kwenda kule kwetu Arusha na Kirimanjaro ni raha tupu! vijana wa leo wanasema ni kugusa tu..

Wasiwasi wangu ni utaratibu mzima ambao serikali imeuweka katika kuhakikisha inailinda miundombinu hiyo. Utaratibu wa kufanya ukarabati mara kwa mara (RPM) nchini ni duni sana. Miundo mbinu ya barabara inaligalimu taifa pesa nyingi sana. Ni haibu kwa nchi kama hii kuona kwamba inao uwezo wa kutoa pesa nyingi kutengeneza barabara ilihali inashindwa kuandaa bajeti ndogo tu ya ukarabati wa barabara zetu.

Usipoziba ufa gharama yake ni kujenga ukuta! Gharama za kujenga ukuta hamna, kwanini msizibe ufa? Viongozi serikalini hili hamlioni? Hau sio vipaumbele kwenu. Nasikitika sana ninapoiangalia barabara ya Mandela ya jijini Dar es salaam. Barabara imechoka sina hamu. Mitaro ya kupitishia maji imeharibika, maji yanaanza kuitafuna barabara. Sasa, nauliza, 'mnasubiri barabara ihishe muanze upya kujenga barabara? Au mnasubiri mradi uongezeke ili muombe pesa nyingi na nyingine mtie kapuni?

Inasikitisha, na inatia asira. Kushinda kufanya ukarabati mdogomdogo mpaka tatizo liwe kubwa ni wizi na ujambazi!

Tubadilike!!!!!

Friday, May 11, 2012

                                         HARAKATI HIZI, NINI MAANAYE?




Asalam aleykum wa ndugu zangu popote mlipo. nimatumaini yangu kuwa mu wazima wa afya. Leo nashika kalamu na karatasi tujadili hili....

Ni hivi karibuni katika chuo chetu cha Ustawi wa jamii tutakuwa na uchaguzi kumtafuta rais mpya chuoni kwetu. Wasiwasi wangu ni harakati za kashifa zinazojitokeza miongoni mwa tuliowengi. Nadhani tumesahau kosa la ushabiki tulilolifanya mwaka jana na kujipatia serikali zembe, hisiyo wajibika na hata hisiyokuwa na huruma kwa wanafunzi wake.

Kama kweli ingekuwa chama cha siasa kingekuwa ndicho kinachomuweka rais wa chuo madarakani basi tungekuwa na jibu moja yakuwa chama tawala hakirudi madarakani. Sasa sio hivyo, ni sera, uungwaji mkono na uwezo wako binafsi katika utendaji wa kazi.

Sio tu chama hicho kilichomuweka rais aliyepo madarakani kingepoteza kura mwaka huu bali hata ndani ya miaka mitatu kisingeweza kujitutumua kusimamisha mgombea kwa kile kilichoonekana kuwa ni udhaifu katika serikari hiyo.

Ndugu, kumpata kiongozi wa kukiongoza chuo sio sawa na kumtafuta kahaba wakati wa shida. Hapa ni vyema kumpima mgombea mwenyewe bila kusikiliza nani anasema nini. Ushabiki, chuki za ovyo zisizokuwa na maslai kwa chuo zisimfanye mtu ausaliti mwaka kwa kuweka pambo madarakani eti ni kiongozi.

Jpime, mpime mwenzio anayekurubuni. Jaribu kujua analolengo gani? Masuala binafsi ya mwenzio yasikupeleke ukaisahau misingi imara ya kumpata kiongozi imara. Watu wanasema dini, wanasema ukabila! Katika jamii za wasomi dini inamaana gani? Kabila lake linatuhusu nini sisi? Kwamba sawa anaweza kuongoza lakini tatizo ni dini yake! Haiji hata kidogo.

Watu wanaleta uchama uchama. Sisi chama cha mtu kinatuhusu nini? Kuna nini mpaka sisi tuanze kuangalia chama cha mtu? Hasa katika jamii ya watu wamoja wasiotengwa na siasa za vyama, kwao siasa za nini?


Kama maneno ya biblia yasemavyo, yatupasa tukumbuke wapi tulikojikwaa tukaanguka.

Jonas John

Wednesday, May 2, 2012

                                            MPAKA LINI?

Nawaza najiwazia,
majibu katu kichwani sipati,
Demokrasia uhuni au mbinu kutuziba midomo,
Aliyeshinda kashindwa aliyeshindwa kashinda.

Mwaka umefika,
chaguzi tumefanya,
wahuni mezani mwakaa,
matokeo kuyaadaa.

Madaraka mwashika,
mwalewa utukufu,
jamii mwaitosa,
hapana watendea haki.

Jamii sasa wazinduka,
Mpango kuwadondosha,
Hilo mwalibaini,
kura mwazipora.

Janja ya nyani,
Hii mwafanya,
jamii itaja kasirika
Nchi mtakimbia.

Jonas John R

Karibuni tutafakari pamoja

Wadau,
Mambo vipi?

Mbele yenu ni blog mpya.  Blogu ambayo imeanzishwa nami mahsusi iwe uwanja wa kutafakari hili na lile katika yale yatuzungukayo kwenye maisha na mahusiano yetu kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kijamii kwa ujumla wake.

Kwa nini Tutafakari?  Kwa nini blog hii iitwe Tutafakari?  Ni kwa kuwa tunapaswa kutafakari, tena si kutafakari peke yake, bali kutafakari kwa kina, kutafakari kwa marefu na mapana juu ya haya mambo yote yatuzungukayo.

Tutafakari.

Tutafakari kwa kuwa tunapotafakari ni dhahiri tunajipa nafasi ya kutafuta majawabu juu ya kadhia zote kwenye maisha yetu.  Tusipotafakari, tuna lipi tutakalojifunza?  Tuna lipi tutakalolitumia kama njia sahihi ya kukabiliana na changamoto zinazotujia kila siku kwenye maisha yetu?  La hasha.  Tusipotafakari, tunajichimbia kaburi la ujinga na umasikini.

Tutafakari.

Hivyo hili ni jukwaa la kutafakari.  Tujadili kwa kina juu ya mustakabali wa taifa letu.

Karibuni sana kwa mchango wa mawazo katika kutafakari.

Tutafakari.  Tutafakari kwa pamoja.

Ahsanteni sana.

Jonas John,
Dar es Salaam, Tanzania.