SIKU HILE IJAYO
Sijui ninini Mungu alimaanisha lakini ukweli ndio huo ya kuwa kwake siku elfu moja ni sawa na siku moja. Kama hivyo ndivyo ilivyo, basi hakuna mtu duniani ambaye aliwai kuishi duniani zaidi ya siku moja. Katika nyakati hizi ambamo shida za dunia zinaweza kumfanya mtu atamani kuukatisha uzima, bado Mungu anaona umeishi nusu siku.
Hachana na hayo. Kwa mwanadamu mambo ni tofauti. Siku njema uisha mapema kabisa na kukuachia maumivu ya kuikumbuka siku hiyo. Mfano; siku ambayo umekutana na marafiki zako wa kitambo. Mnacheka mnapiga soga. Mambo si ndo hayo. Siku hii ingekuwa vyema kama ingerefuka kidogo kuutoa mwanya kwa ndugu hawa kuongea zaidi. Lakini hakuna.
Kadhalika siku mbaya kwa ubaya wake yaweza ikagoma kuisha. Siku moja ikawa kama miaka mia. Jitihada zako za kuitaka siku ikatike mapema zikagonga mwamba. Hilo ndilo jambo baya zaidi japo sina maana ya kuwa kwa Mungu siku zote ni mbaya.
Kadhalika mwaka mmoja waweza kuuona kama miaka elfu ikiwa siku hazijakwendea vyema. Ndiyo, makosa madogo ambayo unaweza kuyafanya mwanzoni mwa mwaka yaweza kufanya mwaka huo uwe mrefu kweli kweli.
Fikiri muhula wa kuchagua viongozi. Kama mtafanya utani na kujipatia viongozi mabuda mwaka huo hakika utakuwa mrefu kwenu maana viongozi watawatia kinyaa.
Sasa hili tunalijua. Huu ni wa kati wa kusema inatosha. Katika jamii yetu ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii tunayo nafasi sasa ya kubadilika. Tusikariri. Kosa tulilolifanya miaka michache iliyopita kujipatia viongozi hewa limetughalimu sana. Sasa ni wakati wa kuangalia utendaji zaidi kuliko mishabiko isiyokuwa na maana yoyote.
Kiongozi bora mwaka huu ni razima ajikane mwenyewe ajitwishe msalaba wake alafu aingie ikulu. Nina maana gani? Kama kuna mtu anataka kuwa kiongozi kwa kusukumwa na watu pasipoyeye kuona ninini anaitaji kuingia madarakani atufanyie, basi hatufai.
Mtu anayegombea ni vyema akawa anatambua ni wapi uongozi huu umevurunda na yeye anataka kuparekebisha. Kama haoni chochote huyo naye ni bomu! Hapana mtu kuingia kwa kisingizio cha kupendekezwa. Huyu akiharibu ataanza kusema kuwa yeye hakuwa tayari kugombea isipokuwa kwa matakwa ya wengine.
Hatumchagi mtu kwa usocial work wake au u-IR wake. Tunayemtaka ni kiongizi wa iswoso. Maana hiyo dhambi ya ubaguzi tutaipeleka wapi. Kwamba japo anaweza lakini tatizo ni IR au social work! Nasema likija hili tena, hatutaliepuka hili la uongozi tulionao. Ni haibu, fedheha na na.. sijui na nini!
Mtu akajiweke katika mizani ajipime mwenyewe. Kugombea sio fashion. Kama huwezi achia wengine. Na kipimo ndo hiki; unajua ni wapi uongozi huu ulikokosea? Je, unayajua matatizo ya chuo chetu? Unajua yakuwa mpaka sasa kuna mfumo tunaoutumia unaokifananisha chuo hiki na chuo cha kata? Kama katika haya unaona maluweluwe hacha kabisa maana hujifai mwenyewe na hutufai sisi.
Jonas R.
No comments:
Post a Comment