Wednesday, September 19, 2012

WALINDE WANAO DHIDI YA MITANDAO MIBOVU

Ukweli: Ingawa watoto wengi wanaopokea ujumbe wa kuwatongoza kwenye mtandao hupuuza au kufuta, unahitaji kuwaelimisha watoto wako kuhakikisha usalama wao.
v  Asilimia 42% ya watoto (umri 10-17) walikiri kuona picha za uchi kwenye mtandao, kwa mujibu wa uchunguzi wa 2005 wa Chuo kikuu cha New Hampshire.
v  Asilimia 66% ya watoto hao hawakufungua viunganishi walivyoviona au kutafuta viunganishi hivyo
v  Mtoto mmoja kati ya saba wenye umri baina ya 10-17 wametongozwa kwenye
mtandao.
v  Asilimia 43% ya utongozaji ulifanywa na watoto wengine chini ya umri wa miaka 18. Asilimia 11% kati ya utongozaji ulifanywa na watu ambao walifahamika tayari kwa walengwa.
  Walinde watoto wako kwa “kuonyesha” na “kuwaambia”

Kuonyesha:
v  Kama unawaruhusu watoto wako kutumia IM, vyumba vya mazungumzo, wasaidie kujiandikisha. Onyesha wasiyostahili kuandika, ili wasitoe habari zao za binafsi? Zungumzia juu ya aina ya mazungumzo yanafaa na yapi yasiyofaa.
    Hakikisha watoto wako wanatumia majina yasiyoelezea jinsia yao kwenye
  mtandao. Waonyeshe mifano ya majina kwenye mtandao ambayo hayafai ( kwa
  mfano: girliegr85 jinsia ya kike)
v  Waonyeshe watoto wako maelezo juu ya watoto wengine ambao wamekuwa
wahanga.
    Kuwaambia:
v  Waambie watoto wako wasijibu jumbe za kuwatongoza na kutoa habari kama kuna mtu anawafuata.
v  Waambie wasijibu barua pepe kutoka kwa watu wasiowafahamu. Ni sawa kutojibu kila barua pepe au mawasiliano.
v  Waambie watoto wasisambaze maelezo juu yao kukiwa pamoja na namba zao za simu na simu za mkononi, anwani, anwani pepe, majina yao kwenye mtandao, picha, shule na mji unakoishi. Eleza kwa nini hii ni ya hatari.
v  Eleza jinsi watu wanavyo”ongopa” kwenye mtandao. Waambie watoto wako kwamba kijana mwenye umri wa “miaka 16” anayetaka kukutana nawe huenda asiwe na umri huo. Anaweza kuwa mtu wa miaka 45 badala yake. Watu pia hudanganya kuwa wa jinsia tofauti kwenye mtandao. Unaweza kuwaonyesha watoto waliokomaa makala kuhusu waviziaji wa watoto wadogo kwenye mtandao wanaojaribu kukutana na watoto kwenyen mtandao kwa ajili ya ngono.
v  Waambie kamwe wasikutane na mtu yeyote ana kwa ana ambaye wamewasiliana kwenye mtandao. Huwezi kujua ni mtu wa aina gani
  (Personal Information) Maelezo ambayo wewe na wanao mnapaswa kuwa waangalifu juu yake kwenye mtandao, kama vile namba za simu za mkononi, barua pepe, jina unalotumia kwenye mtandao, jina la ukoo, anwani, na picha.

KAMA MOSHI UTOWEKAVYO, KADHALIKA SIKU ZANGU ZA KUISHI SI NYINGI

Ni vilio! Wapendwa wetu umewamaliza..! Umewaangamiza kwa maelfu. Umesambaa kama moto wa nyikani. Kifo, kifo.. U nanai wewe? Wapendwa wetu tumewapoteza wengi. Tulio hai tunaishi kwa mashaka! Ndivyo MUNGU MWENYEZI alivyoamua, tuishi kwa wasiwasi. Hili halikuwa pendekezo dogo; "Udongoni ulitoka nawe udongoni utarejea." 


Kwakutaka tuumie zaidi, JEHOVA aliifanya mioyo yetu iwe migumu tusizoee kifo. kila msiba ni mpya na unatisha. Marehemu Ramadhan Ongala maarufu kama Dk Remy Ongala aliwai kuimba ktk moja ya nyimbo zake; Kifo wee kifo, kifo huna uruma. 

BINADAMU kama jani tu, ambalo leo lipo na kesho latupwa motoni. MUNGU tusaidie sisi wanao. Kupitia Baba yetu ADAMU sote tumeukumiwa kifo. Rejea nyuma BABA. Uwepo utofauti kati ya viumbe uliowaumba kwa neno na sisi ulio tutengeneza kwa mfano wako.

Ujana wangu unatoweka kama moshi, na uzee wangu utaulegeza kama tai. SIKU zangu za kuishi umezihesabu, nazo si nyingi. Kira kuchapo ndege wakashangilia kuuona mwanga wa jua mimi uwaza siku zangu zinavyoteketea

Ohh! BWANA; tubariki sisi. Duniani ndimo makazi yetu, waja wako twakulilia.

Jonas John, R.
ISW




Friday, September 14, 2012

MAZINGIRA YA UTENDAJI KAZI POLISI YASIFEDHEHESHWE!

Ni hivi karibuni wananchi tumeshuhudia utendaji kazi mbovu wa jeshi la polisi kwa kuwasulubu raia na pengine kuwaua pasipokuwa na sababu ya kufanya hivyo.

Jeshi la polisi Tanzania sasa limekosa imani kabisa kwa wananchi maana sasa wanaonekana kama wauwaji badala ya walinzi wa amani, wananchi na mali yao.

Kila kona utakakopishana na afande roho juujuu. Kwanini? Hawa ndio wenye stahiki ya kuishi Tanzania kwa kujiamini kuliko wengine? Suala hili halikubaliki hata kidogo! Polisi nani kawafunza kuuwa? Kama ndio hivyo basi wapelekwe Somalia wakalinde amani. Si wanapenda vita!

Orodha ya matukio mabaya yanayousisha mauaji ya polisi inazidi kuongezeka kiasi cha kuitia Doa nchi yetu. Nchi hii ya maziwa na asari sasa imekuwa ni shubiri na mwarobaini kwa makabwela ususan wanapoinua midomo yao kudai haki fulani!

Najua watanzania tumeanza ulevi ususan ulevi wa amani. Baada ya ulevi kipi kinafuata? Ni ugomvi ama vita. Wananchi hatutaki vita japo wakubwa wanaandaa mazingira ya vita.

Pamoja na hayo yote, bado kazi ya polisi ni ya muhimu sana na ya kujitoa katika hii nchi. Jukumu walilopewa la kuhakikisha amani ni jukumu kubwa sana.

Pasiwepo mazingira ya kuwatisha na kuwafanya wafanye kazi katika mazingira ya kutojiamini. Mimi nafurai wanavyokula sahani moja na waarifu. Waarifu wasiotii amri ya jeshi la polisi hatutawatetea kisa wamechapwa na polisi.

Polisi kwakutumia akiri zao sawasawa watambue wapi panafaa kutumia nguvu nyingi, kidogo, wastani au kutotumia nguvu kabisa.

Na hao vigogo wanaowaagiza polisi kuuwa wakati wao wako ofisini ni hatari! Mnawatia polisi dosari kwa maslahi yenu.

Nashauri polisi wetu wapewe elimu ya uraia ili wajuwe jinsi ya kufanya kazi na jamii.
seniour Josy