Wednesday, September 19, 2012

KAMA MOSHI UTOWEKAVYO, KADHALIKA SIKU ZANGU ZA KUISHI SI NYINGI

Ni vilio! Wapendwa wetu umewamaliza..! Umewaangamiza kwa maelfu. Umesambaa kama moto wa nyikani. Kifo, kifo.. U nanai wewe? Wapendwa wetu tumewapoteza wengi. Tulio hai tunaishi kwa mashaka! Ndivyo MUNGU MWENYEZI alivyoamua, tuishi kwa wasiwasi. Hili halikuwa pendekezo dogo; "Udongoni ulitoka nawe udongoni utarejea." 


Kwakutaka tuumie zaidi, JEHOVA aliifanya mioyo yetu iwe migumu tusizoee kifo. kila msiba ni mpya na unatisha. Marehemu Ramadhan Ongala maarufu kama Dk Remy Ongala aliwai kuimba ktk moja ya nyimbo zake; Kifo wee kifo, kifo huna uruma. 

BINADAMU kama jani tu, ambalo leo lipo na kesho latupwa motoni. MUNGU tusaidie sisi wanao. Kupitia Baba yetu ADAMU sote tumeukumiwa kifo. Rejea nyuma BABA. Uwepo utofauti kati ya viumbe uliowaumba kwa neno na sisi ulio tutengeneza kwa mfano wako.

Ujana wangu unatoweka kama moshi, na uzee wangu utaulegeza kama tai. SIKU zangu za kuishi umezihesabu, nazo si nyingi. Kira kuchapo ndege wakashangilia kuuona mwanga wa jua mimi uwaza siku zangu zinavyoteketea

Ohh! BWANA; tubariki sisi. Duniani ndimo makazi yetu, waja wako twakulilia.

Jonas John, R.
ISW




No comments:

Post a Comment