Friday, September 14, 2012

MAZINGIRA YA UTENDAJI KAZI POLISI YASIFEDHEHESHWE!

Ni hivi karibuni wananchi tumeshuhudia utendaji kazi mbovu wa jeshi la polisi kwa kuwasulubu raia na pengine kuwaua pasipokuwa na sababu ya kufanya hivyo.

Jeshi la polisi Tanzania sasa limekosa imani kabisa kwa wananchi maana sasa wanaonekana kama wauwaji badala ya walinzi wa amani, wananchi na mali yao.

Kila kona utakakopishana na afande roho juujuu. Kwanini? Hawa ndio wenye stahiki ya kuishi Tanzania kwa kujiamini kuliko wengine? Suala hili halikubaliki hata kidogo! Polisi nani kawafunza kuuwa? Kama ndio hivyo basi wapelekwe Somalia wakalinde amani. Si wanapenda vita!

Orodha ya matukio mabaya yanayousisha mauaji ya polisi inazidi kuongezeka kiasi cha kuitia Doa nchi yetu. Nchi hii ya maziwa na asari sasa imekuwa ni shubiri na mwarobaini kwa makabwela ususan wanapoinua midomo yao kudai haki fulani!

Najua watanzania tumeanza ulevi ususan ulevi wa amani. Baada ya ulevi kipi kinafuata? Ni ugomvi ama vita. Wananchi hatutaki vita japo wakubwa wanaandaa mazingira ya vita.

Pamoja na hayo yote, bado kazi ya polisi ni ya muhimu sana na ya kujitoa katika hii nchi. Jukumu walilopewa la kuhakikisha amani ni jukumu kubwa sana.

Pasiwepo mazingira ya kuwatisha na kuwafanya wafanye kazi katika mazingira ya kutojiamini. Mimi nafurai wanavyokula sahani moja na waarifu. Waarifu wasiotii amri ya jeshi la polisi hatutawatetea kisa wamechapwa na polisi.

Polisi kwakutumia akiri zao sawasawa watambue wapi panafaa kutumia nguvu nyingi, kidogo, wastani au kutotumia nguvu kabisa.

Na hao vigogo wanaowaagiza polisi kuuwa wakati wao wako ofisini ni hatari! Mnawatia polisi dosari kwa maslahi yenu.

Nashauri polisi wetu wapewe elimu ya uraia ili wajuwe jinsi ya kufanya kazi na jamii.
seniour Josy

1 comment: