Friday, May 11, 2012

                                         HARAKATI HIZI, NINI MAANAYE?




Asalam aleykum wa ndugu zangu popote mlipo. nimatumaini yangu kuwa mu wazima wa afya. Leo nashika kalamu na karatasi tujadili hili....

Ni hivi karibuni katika chuo chetu cha Ustawi wa jamii tutakuwa na uchaguzi kumtafuta rais mpya chuoni kwetu. Wasiwasi wangu ni harakati za kashifa zinazojitokeza miongoni mwa tuliowengi. Nadhani tumesahau kosa la ushabiki tulilolifanya mwaka jana na kujipatia serikali zembe, hisiyo wajibika na hata hisiyokuwa na huruma kwa wanafunzi wake.

Kama kweli ingekuwa chama cha siasa kingekuwa ndicho kinachomuweka rais wa chuo madarakani basi tungekuwa na jibu moja yakuwa chama tawala hakirudi madarakani. Sasa sio hivyo, ni sera, uungwaji mkono na uwezo wako binafsi katika utendaji wa kazi.

Sio tu chama hicho kilichomuweka rais aliyepo madarakani kingepoteza kura mwaka huu bali hata ndani ya miaka mitatu kisingeweza kujitutumua kusimamisha mgombea kwa kile kilichoonekana kuwa ni udhaifu katika serikari hiyo.

Ndugu, kumpata kiongozi wa kukiongoza chuo sio sawa na kumtafuta kahaba wakati wa shida. Hapa ni vyema kumpima mgombea mwenyewe bila kusikiliza nani anasema nini. Ushabiki, chuki za ovyo zisizokuwa na maslai kwa chuo zisimfanye mtu ausaliti mwaka kwa kuweka pambo madarakani eti ni kiongozi.

Jpime, mpime mwenzio anayekurubuni. Jaribu kujua analolengo gani? Masuala binafsi ya mwenzio yasikupeleke ukaisahau misingi imara ya kumpata kiongozi imara. Watu wanasema dini, wanasema ukabila! Katika jamii za wasomi dini inamaana gani? Kabila lake linatuhusu nini sisi? Kwamba sawa anaweza kuongoza lakini tatizo ni dini yake! Haiji hata kidogo.

Watu wanaleta uchama uchama. Sisi chama cha mtu kinatuhusu nini? Kuna nini mpaka sisi tuanze kuangalia chama cha mtu? Hasa katika jamii ya watu wamoja wasiotengwa na siasa za vyama, kwao siasa za nini?


Kama maneno ya biblia yasemavyo, yatupasa tukumbuke wapi tulikojikwaa tukaanguka.

Jonas John

No comments:

Post a Comment