Salaamu sana ndugu zangu nikitambua fika yakuwa mnaendelea na kazi nzito ya kulijenga taifa letu hili changa la Tanzania. Mimi leo nawajia, nakuja na hili.
Tujikumbushe story ya zamani tuliyoisoma tukiwa drs la pili hivi. Story hii inamuhusu popo. Swali ni je, popo ni ndege ama mnyama. Mwisho wa kigano hiki ntakutaka kunijibu swali hili.
POPO NI NDEGE?
Hapo zamani za kale wanyama wote waliishi mstuni. Binadamu aliishi peke yake huko kwenye makazi yake mbali na hao wanyama. Kila mara binadamu alikwenda mstuni kuwinda wanyama na ndege kwa ajili ya kujipatia kitoweo. Tabia hii ya binadamu ya kuwaua ndege hovyo na wanyama iliwakasilisha sana wanyama hao wakazi wa mstuni.
Wanyama kwa pamoja waliazimia kukutana kuweka mikakati kwa ajiri ya kuikomesha tabia hatarishi ya binadamu. Ndege nao wala hawakubaki nyuma. Nao walianzisha vikao vilivyokuwa na maana moja ya kumsambaratisha binadamu.
Wanyama walianzisha vikao kwa nguvu zote. Wakawekeana maazimio na mikakati ya kuhakikisha mwanadamu hagusi tena himaya ya wanyama hao. Sungura alifuatia baada ya kongoni kumaliza maongezi yake. Sungura akaanza kwa kusema; "ndugu zanguni, najuwa nyote mnajua fika yakuwa ndugu zetu wengi wameishia mikononi mwa mwanadamu na kugeuzwa kitoweo." Sungura aligeuka kushoto kisha kulia. "Amini msiamini jukumu la kumshinda mwanadamu ni letu sote pasipo kumbagua mtu. Wakale walisema umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Kama hatutatafakari vyema ya wahenga tutaishia kuwa supu katika bakuli la mwanadamu. Mimi ninalo wazo," "mh!" wanyama wote waliitikia kisha sungura akaendelea; "Nadhani ndugu zanguni tukienda kuhemea huku na kule tusiende tofauti. Twende kwa umoja wetu. Tena yatupasa tutengeneze filimbi kila mmoja wetu awe nayo. Popote mwenzetu atakapomwona mwanadamu basi apulize kipenga nasi tutajua hatari inayotukabiri." Alimaliza sungura mazungumuzo yake na kuketi chini.
Wanyama wote waliafikiana na wazo la sungura na kuazimia kumtafuta mtaalamu wa kutengeneza filimbi hizo. Wanyama wote walitawanyika na kuagana kila mtu akienda kuzitekeleza kazi za siku. Kuutafuta mkate wa kilasiku wa kwao pamoja na watoto wao.
Huku mkutano wa wanyama ukiendelea, ndege nao hawakubaki nyuma. Mkutano wao ulifanyika juu ya mbuyu. Ndege wote waliitikia mwito wa mwenyekiti wao mh. Mbuni. Lamgambo lilipolia, ndege wakazitanda mbawa zao juu ya hanga mbio kuelekea eneo la tukio.
Popo naye akajifunga kibwebwe kuelekea kunako mbuyu. Hakutaka hili la leo limpite. Haraka haraka akajichanganya na wenzie.
Mkutano ukaanza. Mwenyekiti alianza kwa kuwakaribisha ndege wote, popo naye yu miongoni mwao. Baadae akatoa fursa kwa ndege wengine kutoa mawazo katika mchakato wa kumkabiri adui yao.
Kanga alikuwa wa kwanza kuinuka. Baada ya kuzikunguta mbawa zake, kanga alianza kwa kusema; "ndugu zaangini mliopo mahali hapa. Natumai sote tunaguswa na tatizo hili zito. Mwanadamu ametufanya chakula kitamu kwake. Ama hakika, yatufaa tumshinde na siraha yetu kuu ni umoja. Tukiwa wamoja kila kitu kitawezekana. Mimi niseme yakuwa itakuwa vyema kama sote tutaungana na kuitetea haki yetu." alimaliza kanga. Sasa ilikuwa zamu ya popo kuongea. Pasipo kujua kuwa anachunguzwa akaanza kupayuka. Maneno yake hayakuwaingia ndege wengine. Ndege wakaanza kujiuliza maswali, huyu jamaa sio mwenzetu au? Mbona ana meno? Lakini mbona ana mabawa na anapaa!
Baadae njiwa akona isiwe tabu. Akamuuliza swali. "Samahani, mbona wewe una meno? Yamkini wewe utakuwa mnyama! Hapa hutufai. Popo akajitetea sana lakini lo! Ndege walisha mwondolea imani, wakamfukuza.
Popo akaona isiwe tabu, maadamu yeye ni mnyama basi ataudhulia vikao vya wanyama. Siku ya kikao cha wanyama ikafika. Wanyama wakakusanyika chini ya mti wa mwembe. Wakiwa wanaendelea, popo naye akajichanganya. Wanyama wakataharuki. Iweje ndege audhulie vikao vyao! Wakamfukuza. Akajitetea sana. Akasema pamoja na kuwa ana mabawa lakini bado ni mnyama maana anyo meno kama wao na anazaa kiumbe kamili. Neno la mwisho alilimaliza na kofi kali kutoka kwa mzee simba aliyekuwa kagathabishwa na maneno ya popo. Popo aliona nyota tu. Akatimuka mbio kuelekea kwake na kwa aibu akaapa kutotembea mchana. Yeye akapanga mipango yake ataifanya usiku kufuta haibu iliyompata.
Adi leo popo ujificha mchana na kutoka usiku kutafuta chakula. Hii si kwasababu popo anapenda bali hali iliyomsibu.
Hadithi hii inanifundisha nini? Mtu naye anaweza kuwa kama popo. Asiwe mnyama wala ndege! Dunia hii kweli ni hatari.
Kitu gani kinatufanya tupoteze mwelekeo na kutokuwa na upande kama popo? Watu tunakuwa kama bendera. Upepo ukipepea kuelekea kusini nawewe kusini, ukigeuzia mashariki nawewe mashariki. Sasa tofauti kati ya m2 wa namna hii na demu ambaye kwa muda umpenda huyu lakini akiona mwenye mali zaidi ugeuza maamuzi yake iko wapi?.
Ndugu zanguni, ndugu wa damu, BIRA II. Tatizo sio usisi, tatizo ni sisi. Wana BIRA II, mioyo ya unafiki hatuijui? Mbona tunaangaika kutakatisha kaniki wakati rangi yake tunaijua?
Zimeanza kuwepo taarifa kuwa kitakacho tudondosha BIRA II katika mbio za urais ni moyo wa usisi uliojengeka miongoni mwa wanafunzi tulio wengi. Hili nalikataa kwa herufi kubwa. Sio kweli hata kidogo. Hii ilikuwa mikakati tuliyojiwekea kama darasa kuhakikisha tunashinda chaguzi zijazo. Haukuwa usisi bali uungaji mkono wagombea watakaojitokeza drsn kwetu.
Tatizo limekuja kuwa ni unafiki, ushushushu wa kupeleka habari za ndani za darasa nje ya darasa kinyume ya utaratibu na makubaliano. Ujuaji unazidi kututafuna taratibu kama mchwa! Naikumbuka kauli moja aliyoitoa SAMWELI darasani kipindi fulani na namnukuu; "tatizo ni hilo. Umu ndani kunawatu wanaodhani kuwa kuna watu waliokuja kusoma na waliokuja kuongoza. Kwa upumbavu huu tutabakia kuwapigia kura wenzetu na kuwapigia makofi. ISOSWO tuzidi kuisikia tu. Na kama kulikuwa na wakati mzuri wa sisi kuingia madarakani ulikuwa ni mwaka huu." mwisho wa kumnukuu.
Haya maneno hayajachuja. Katika unafiki wa namna hii, hatuwezi kamwe kuitawala isoswo. MWENYEZI MUNGU katika kitabu cha Ufunuo anasema dhairi yakuwa hataki watu wa uvuguvugu. Kama ukiamua kuwa wa moto basi kuwa wa moto kabisa na kama ukiamua kuwa wa baridi uwe wa baridi kwelikweli.
Ukweli ni hivi, hata mimi nawachukia watu wa uvuguvugu. Kama kweli we ni wa moto basi kuwa wa vile.
Ndugu zanguni, usisi ni suala linalofaa kupigwa vita ila umoja wetu kama BIRA II ubaki palepale. Mimi nimesema hayo. Wadau ni ninyi. Ni bora kukaa kimya kuliko kujibu swali tusilolijua. Darasa ni sisi na sisi ni darasa. Uhai wa darasa uko mikononi mwetu. Tuubinye ufe au tuuachie uruke. TATIZO SIO USISI, TATIZO NI SISI.
By Jonas John R.