Tuesday, July 31, 2012

WANA HABARI KAMA HAMJUI SHERIA KAENI KIMYA.

VYOMBO VYA HABARI NI KERO MGOMO WA WALIMU

Kila mtu na weledi wake. Taaluma ni kitu cha msingi sana. Kila mtu ni mjuzi katika fani aliyoisomea. Na leo hii ndio maana kuna mgawanyo wa kazi. Sio kila mtu afanye kazi zote.

Mwalimu akafundishe, mwana habari akatupashe habari, wanasiasa wakatudanganye, nakadhalika, nakadhalika.

Sote tunajua ambavyo walimu wamekuwa katika mgogoro wa kimaslahi na serikali uliowapelekea kugoma hivi juzi. Walimu hawa watakuwa halari kugoma iwapo wametimiza matakwa ya mgomo harali kama yalivyoainishwa katika sheria ya kazi na mahusiano kazini ya mwaka 2004, no 6 katika kifungu cha 80(1) (a)-(e).

Sheria hii pia katika kifungu cha 86(7)(a) kinataja wazi uhuru wa wafanyakazi kugoma iwapo CMA wameshindwa kutatua mgogoro wao wa kimaslahi.

Katika sheria hii hamna sehemu ilikoruhusiwa mgogoro wa kimaslahi kuupeleka mahakamani au kwa mtatuzi yaani Arbitrator. Kitendo cha Serikali kuamua kuupeleka mgomo wa wlimu mahakamani ni udhaifu na ni kudhiirisha kushindwa kwa serikali na kutapatapa.

Sasa kinachonitia wazimu hadi kichefuchefu ni hawa waandishi wa habari wasiojua chochote kuhusu migogoro na sheria mahala pa kazi kujitia kimbelembele kukosoa juhudi za walimu kudai haki zao.

Waandishi wa habari na watangazaji sijui kama wanaijua vema sheria ya kazi! Utasikia wakisema walimu wamo katika mgomo usio halari! Nani kasema si halari? Je, uhalari wa mgomo unategemea sheria au jinsi wewe unavyowaza!

Hacheni ushabiki na ukibaraka wa mambo msiyoyajua. Mahakama pekee ndiyo itasema iwapo mgomo ulikuwa harali au la lakini sio wewe uliyelala ukaamuka na mawazo yako ukatutangazia.

Kufanya kazi katika mazingira magumu, ujira mdogo, sheria ngumu za kazi na ubabe katika mazingira ya kazi havina budi kupingwa kwa nguvu zote n a kila mtanzania mwenye kutaka maendeleo.

Heko walimu, umoja, nguvu, pamoja.

Sunday, July 29, 2012

KATIKA HILI MANAGEMENT TAASISI YA USTAWI WA JAMII HAMKUFIKIRIA

ADA TAASISI YA USTAWI WA JAMII NI KUZUNGUMKUTI CHA FADHILI

Nilipopewa prospectus kwa mara ya kwanza kabisa hivi majuzi, haraka nikazikimbilia kurasa zenye kuonesha mpangilio wa ada kwa mwaka huu. Nilishutuka sana. Niliona kuwa mfumuko wa bei sasa umeingilia hata ada.

Nilisikitika kuona kwamba management kwa kusaidiana na bodi ya ukurugenzi wameamua kupandisha michango chuoni hapo kwa takribani asilimia elfu moja (1000%).

Gharama ya usajiri imepanda toka Tsh 5000/- adi Tsh 50,000/-, fomu za maombi ya kujiunga zimepanda kutoka Tsh 30,000/- adi Tsh 50,000/-, kitambulisho kimepanda toka Tsh 5000/- adi Tsh 15,000/-, ada ya hostel sasa ni shilingi 400,000 kutoka 250,000 ya zamani.

Ni vi tuko. Kwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu ngazi ya shaada ya kwanza atarazimika kulipa shilingi milioni mbili na nusu (2,500,000) kama ada ya mwaka kutoka milioni moja na elfu mbili (1,002,000) malipo ya zamani.

Mbaya zaidi ni kwa mwanafunzi anayeomba kuhairisha mtiani kwa sababu zinazoweza kumzuia kufanya mtihani kwa utulivu huyu atarazimika kulipa shilingi laki moja (100,000) kwa ajiri ya kukubaliwa ombi lake.
Mtihani wa mwisho wa semester tangu sasa utakuwa ukilipiwa shilingi elfu sabini (70000).

Hapo ndipo nilipoona Taasisi imechoka. Wapo watu wanaoshindwa kulipa ada ya semester na hivyo kutoruhusiwa kufanya mtihani, leo hii mnasema hata mtihani tunaulipia! Haya ndio maajabu ya Taasisi.

Katika mfumo wa vyuo vikuu tanzania, na taasisi za elimu ya juu nchini, ni Taasisi ya Ustawi wa Jamii  pekee inayotoza ada kubwa kwa mwaka kwa mpango wa sasa.

Chuo hiki ambacho bodi ya mikopo wamekiondolea udhamini wa mkopo sasa mnataka mtu alete miliono mbili na nusu! Aitoe wapi? Hiki ni chuo cha serikali chenye udhamini wa serikali kwa asilimia kadhaa sasa mbona mnatutupia zigo zito lililojaa misumari inayochoma!

Sasa mwanafunzi atalazimika kukilipa chuo shilingi laki mbili (200,000) kama ela ya Field Work Practice na shilingi laki nne (400,000) kama ela ya research!

 Hivi bodi ni watu au mashine? Wanafahamu uchungu na ugumu wa maisha? Mbona wanatutesa hivi? Kama bodi haipo kwa maslahi ya wanafunzi na mstakabali wao basi haitufai!

Leo parking ni shlingi 2000. Si kwamba nalalamika kwasababu nina gari. La! Asha! Hii ni pesa nyingi. Tangu lini mtu akalipia parking ya nyumbani au eneo ulikoenda kununua huduma.

Nijukumu la Taasisi kutafutia wateja wake parking na sio kuwatoza pesa zote hizo.

Mimi nashauri michango isiyokuwa na msingi iondolewe ili kuwapa wanafunzi hauweni. Uhai wa Taasisi u mikononi mwetu na kwa namna hii taasisi tutaizika.

NIDA WAMEKURUPUKA KATIKA ZOEZI LA VITAMBULISHO VYA TAIFA

KATIKA ZOEZI ZIMA LA VITAMBULISHO VYA UTAIFA, NIDA MMEKURUPUKA.


Ni hivi karibuni ambapo taifa letu limeingia katika mchakato wa kutoa vitambulisho vya utaifa kwa wakazi wote nchini na watanzania wote.

Zoezi hili linasimamiwa na taifa chini ya wakala wa vitambulisho vya taifa NIDA. Kusema kweli NIDA wamekurupuka katika kuanzisha utekelezaji wa mpango huu wakianza na mkoa wa Dar es salaam. Pamoja na yakuwa siku walizotoa hapo hawali kutotosha bado NIDA hawakufanya tathmini ya hawali kujua idadi ya wakazi katika vitongoji vya mkoa huu.

Zipo sehemu zenye wakazi wengi kupindukia na bado wameweka kituo kimoja cha kuandikia watu katika kata moja. Hili limezua fujo katika vituo hivyo watu wakigombea kuandikwa. Wakazi wa jiji la Dar es salaamu kwa siku kadhaa sasa wameailisha shughuli zao za msingi wakishinda katika mistari wakingoja kuandikwa.

Aidha, mbali na kuwa vituo vya uandikishaji kufunguliwa asubuhi ya saa mbili, watu wamekuwa wakifurika vituoni hapo tangu saa kumi usiku kuwai kile wanachokiita namba.

Pamoja na adha hii, bado kumekuwa na utaratibu mbovu unaoshindwa kuwabaini watu waliowai. Hali hii imesababisha watu kutumia nguvu zaidi katika zoezi hili badala ya utaratibu na utu.

Zoezi hili limeonekana pia kuvutia rushwa kwa watendaji na kutoa huduma kulingana na mtu anavyojulikana.

Ni ombi langu sasa NIDA watakapokuwa wameamishia zoezi hili mikoani wajitaidi kuboresha huduma zao ikiwa ni pamoja na kuweka ulinzi vituoni kulinda usalama wa raia. Pia NIDA wajaribu kufikiria uwezekano wa kuandikishwa na kupiga picha kwa wakati mmoja. Mbali na kwamba zoezi hilo litaokoa muda bado gharama za uendeshaji na usumbufu vitapungua.

Niseme, vitambulisho vya utaifa ni suala la maana sana. Ni vyema kila raia kujiandikisha kupata utambulisho huu. Utaratibu ubooreshwe ili kutoa mwanya kwa watu wengi kujiandikisha. Vituo vya kujiandikisha viwekwe vingi kulingana na uwingi wa watu wa eneo.

Saturday, July 7, 2012

                          MCHAGUE FRANK JOHN KWA MAENDELEO YA ISWOSO.


Twendako sio mbali. Sio mbali hata kidogo. Ni punde tu!

Naliposema BIR II tushikamane nilimaanisha hili. Sasa yametimia.

Ndugu yetu, mwenzetu ndg Frank John anawania kinyang'anyiro katika harakati za kuitwa raisi wa iswoso. Akiwa na kauri mbiu yake naamini kijana amekuja kutatua matatizo ya walio wengi.

Kama nilivyowai kuandika katika mtandao huu, natumai kijana anajua ni kwanini anaitaji kuingia ISWOSO. Madhaifu na mapungufu yaliyooneshwa na serikali dhaifu inayomaliza muda wake hayafai tena kujirudia.

Frank ni mfananishe na sauti iliayo nyikani, itengenezeni njia yake, yanyosheni mapito yake, kila bonde na lijazwe, na mashimo yafukiwe ili kijana aingie Ikulu.

Ndugu zanguni, hatutamchagua Frank kwasababu yeye ni IR bali kwa uweza wake mkubwa wa kutenda shughuli mbalimbali.

Ni dhairi yakuwa kijana amekuwa akijituma sana katika kuakikisha gurudumu la maendeleo ya chuo chetu likienda mbele. Amekuwa wa kwanza katika kufuatilia mikopo huku akijitoa mhanga hata kulikosa  darasa kwa kufuatilia mambo yanayotuhusu sote.

Ni upendo wa hajabu huu ambao mtu anakuwa tayari kujitoa mwenyewe kwa ajiri ya watu walio wengi. Huyu ndiye yule anayetufaa.  Hiyo ndiyo nyota ya mashariki waliyoiona mama jusi nyakati za mfalme Helode.

Tuziweke kando tofauti zetu za course na kumchagua mtu afaaye. Hebu tuvunje mwiko. Tuamini inawezekana. Mabadiliko ni muhimu na yanaanza na sisi.

MCHAGUE FRANK JOHN KWA MAENDELEO YA CHUO CHETU