ADA TAASISI YA USTAWI WA JAMII NI KUZUNGUMKUTI CHA FADHILI
Nilipopewa prospectus kwa mara ya kwanza kabisa hivi majuzi, haraka nikazikimbilia kurasa zenye kuonesha mpangilio wa ada kwa mwaka huu. Nilishutuka sana. Niliona kuwa mfumuko wa bei sasa umeingilia hata ada.
Nilisikitika kuona kwamba management kwa kusaidiana na bodi ya ukurugenzi wameamua kupandisha michango chuoni hapo kwa takribani asilimia elfu moja (1000%).
Gharama ya usajiri imepanda toka Tsh 5000/- adi Tsh 50,000/-, fomu za maombi ya kujiunga zimepanda kutoka Tsh 30,000/- adi Tsh 50,000/-, kitambulisho kimepanda toka Tsh 5000/- adi Tsh 15,000/-, ada ya hostel sasa ni shilingi 400,000 kutoka 250,000 ya zamani.
Ni vi tuko. Kwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu ngazi ya shaada ya kwanza atarazimika kulipa shilingi milioni mbili na nusu (2,500,000) kama ada ya mwaka kutoka milioni moja na elfu mbili (1,002,000) malipo ya zamani.
Mbaya zaidi ni kwa mwanafunzi anayeomba kuhairisha mtiani kwa sababu zinazoweza kumzuia kufanya mtihani kwa utulivu huyu atarazimika kulipa shilingi laki moja (100,000) kwa ajiri ya kukubaliwa ombi lake.
Mtihani wa mwisho wa semester tangu sasa utakuwa ukilipiwa shilingi elfu sabini (70000).
Hapo ndipo nilipoona Taasisi imechoka. Wapo watu wanaoshindwa kulipa ada ya semester na hivyo kutoruhusiwa kufanya mtihani, leo hii mnasema hata mtihani tunaulipia! Haya ndio maajabu ya Taasisi.
Katika mfumo wa vyuo vikuu tanzania, na taasisi za elimu ya juu nchini, ni Taasisi ya Ustawi wa Jamii pekee inayotoza ada kubwa kwa mwaka kwa mpango wa sasa.
Chuo hiki ambacho bodi ya mikopo wamekiondolea udhamini wa mkopo sasa mnataka mtu alete miliono mbili na nusu! Aitoe wapi? Hiki ni chuo cha serikali chenye udhamini wa serikali kwa asilimia kadhaa sasa mbona mnatutupia zigo zito lililojaa misumari inayochoma!
Sasa mwanafunzi atalazimika kukilipa chuo shilingi laki mbili (200,000) kama ela ya Field Work Practice na shilingi laki nne (400,000) kama ela ya research!
Hivi bodi ni watu au mashine? Wanafahamu uchungu na ugumu wa maisha? Mbona wanatutesa hivi? Kama bodi haipo kwa maslahi ya wanafunzi na mstakabali wao basi haitufai!
Leo parking ni shlingi 2000. Si kwamba nalalamika kwasababu nina gari. La! Asha! Hii ni pesa nyingi. Tangu lini mtu akalipia parking ya nyumbani au eneo ulikoenda kununua huduma.
Nijukumu la Taasisi kutafutia wateja wake parking na sio kuwatoza pesa zote hizo.
Mimi nashauri michango isiyokuwa na msingi iondolewe ili kuwapa wanafunzi hauweni. Uhai wa Taasisi u mikononi mwetu na kwa namna hii taasisi tutaizika.
No comments:
Post a Comment