MCHAGUE FRANK JOHN KWA MAENDELEO YA ISWOSO.
Twendako sio mbali. Sio mbali hata kidogo. Ni punde tu!
Naliposema BIR II tushikamane nilimaanisha hili. Sasa yametimia.
Ndugu yetu, mwenzetu ndg Frank John anawania kinyang'anyiro katika harakati za kuitwa raisi wa iswoso. Akiwa na kauri mbiu yake naamini kijana amekuja kutatua matatizo ya walio wengi.
Kama nilivyowai kuandika katika mtandao huu, natumai kijana anajua ni kwanini anaitaji kuingia ISWOSO. Madhaifu na mapungufu yaliyooneshwa na serikali dhaifu inayomaliza muda wake hayafai tena kujirudia.
Frank ni mfananishe na sauti iliayo nyikani, itengenezeni njia yake, yanyosheni mapito yake, kila bonde na lijazwe, na mashimo yafukiwe ili kijana aingie Ikulu.
Ndugu zanguni, hatutamchagua Frank kwasababu yeye ni IR bali kwa uweza wake mkubwa wa kutenda shughuli mbalimbali.
Ni dhairi yakuwa kijana amekuwa akijituma sana katika kuakikisha gurudumu la maendeleo ya chuo chetu likienda mbele. Amekuwa wa kwanza katika kufuatilia mikopo huku akijitoa mhanga hata kulikosa darasa kwa kufuatilia mambo yanayotuhusu sote.
Ni upendo wa hajabu huu ambao mtu anakuwa tayari kujitoa mwenyewe kwa ajiri ya watu walio wengi. Huyu ndiye yule anayetufaa. Hiyo ndiyo nyota ya mashariki waliyoiona mama jusi nyakati za mfalme Helode.
Tuziweke kando tofauti zetu za course na kumchagua mtu afaaye. Hebu tuvunje mwiko. Tuamini inawezekana. Mabadiliko ni muhimu na yanaanza na sisi.
MCHAGUE FRANK JOHN KWA MAENDELEO YA CHUO CHETU
No comments:
Post a Comment