Wadau,
Mambo vipi?
Mbele yenu ni blog mpya. Blogu ambayo imeanzishwa nami mahsusi iwe uwanja wa kutafakari hili na lile katika yale yatuzungukayo kwenye maisha na mahusiano yetu kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kijamii kwa ujumla wake.
Kwa nini Tutafakari? Kwa nini blog hii iitwe Tutafakari? Ni kwa kuwa tunapaswa kutafakari, tena si kutafakari peke yake, bali kutafakari kwa kina, kutafakari kwa marefu na mapana juu ya haya mambo yote yatuzungukayo.
Tutafakari.
Tutafakari kwa kuwa tunapotafakari ni dhahiri tunajipa nafasi ya kutafuta majawabu juu ya kadhia zote kwenye maisha yetu. Tusipotafakari, tuna lipi tutakalojifunza? Tuna lipi tutakalolitumia kama njia sahihi ya kukabiliana na changamoto zinazotujia kila siku kwenye maisha yetu? La hasha. Tusipotafakari, tunajichimbia kaburi la ujinga na umasikini.
Tutafakari.
Hivyo hili ni jukwaa la kutafakari. Tujadili kwa kina juu ya mustakabali wa taifa letu.
Karibuni sana kwa mchango wa mawazo katika kutafakari.
Tutafakari. Tutafakari kwa pamoja.
Ahsanteni sana.
Jonas John,
Dar es Salaam, Tanzania.
Hongera sana mkuu kwa hatua hii. Nafurahi sana kuona vijana tunaacha kulala na kulalamika, badala yake tunashiriki kikamilifu katika kuutafakari mustakabali wa taifa letu.
ReplyDeleteKaribu sana katika ulimwengu wa kublog.