TANZANIA NA RPM
Tanzania ni moja wapo ya nchi zinazoendelea. Hapana shaka ya kwamba katika kufikia miamoja utaanza na moja. Tangu tujipatie uhuru mwaka 1961, Tanzania imekuwa ikifanya jitihada za makusudi kuhakikisha maendeleo yanafikiwa kwa kutumia rasilimali zetu tulizo nazo.
Naamini kwa kiwango tulichofikia kinaelekea kutia moyo hususan kwa mwananchi anayeitakia maendeleo nchi hii. Kwa muda wa takriban miaka 50 ya uhuru, Tanzania imejitutumua na kujaribu kushughulika kwa sana kuwaletea wananchi maendeleo.
Tanzania ya sasa imejenga barabara nzuri za kusifika. Maeneo mengi ya nchi yetu sasa yanafikika ki urahisi kwa sababu ya ubora wa miundo mbinu tuliyonayo ususan barabara. Leo ni rahisi kwa mtu kusafiri kutoka Dar es salaam hadi kigoma kwa siku mbili tu mwendo wa basi. Tofauti na zamani ambapo ilikuwa ikimrazimu mtu kusafiri kwa takribani siku nne hadi tano kuitafuta Kigoma.
Dar es salaam hadi Mbeya kwetu wanasema 'kachwant'apasi'. Ninamaana gani? Leo waweza kutoka Dar kwenda kunywa chai Mbeya na kurudi Dar ukaendelea na zako shughuli. Vivyo hivyo hata kwenda kule kwetu Arusha na Kirimanjaro ni raha tupu! vijana wa leo wanasema ni kugusa tu..
Wasiwasi wangu ni utaratibu mzima ambao serikali imeuweka katika kuhakikisha inailinda miundombinu hiyo. Utaratibu wa kufanya ukarabati mara kwa mara (RPM) nchini ni duni sana. Miundo mbinu ya barabara inaligalimu taifa pesa nyingi sana. Ni haibu kwa nchi kama hii kuona kwamba inao uwezo wa kutoa pesa nyingi kutengeneza barabara ilihali inashindwa kuandaa bajeti ndogo tu ya ukarabati wa barabara zetu.
Usipoziba ufa gharama yake ni kujenga ukuta! Gharama za kujenga ukuta hamna, kwanini msizibe ufa? Viongozi serikalini hili hamlioni? Hau sio vipaumbele kwenu. Nasikitika sana ninapoiangalia barabara ya Mandela ya jijini Dar es salaam. Barabara imechoka sina hamu. Mitaro ya kupitishia maji imeharibika, maji yanaanza kuitafuna barabara. Sasa, nauliza, 'mnasubiri barabara ihishe muanze upya kujenga barabara? Au mnasubiri mradi uongezeke ili muombe pesa nyingi na nyingine mtie kapuni?
Inasikitisha, na inatia asira. Kushinda kufanya ukarabati mdogomdogo mpaka tatizo liwe kubwa ni wizi na ujambazi!
Tubadilike!!!!!
No comments:
Post a Comment