Wednesday, May 2, 2012

                                            MPAKA LINI?

Nawaza najiwazia,
majibu katu kichwani sipati,
Demokrasia uhuni au mbinu kutuziba midomo,
Aliyeshinda kashindwa aliyeshindwa kashinda.

Mwaka umefika,
chaguzi tumefanya,
wahuni mezani mwakaa,
matokeo kuyaadaa.

Madaraka mwashika,
mwalewa utukufu,
jamii mwaitosa,
hapana watendea haki.

Jamii sasa wazinduka,
Mpango kuwadondosha,
Hilo mwalibaini,
kura mwazipora.

Janja ya nyani,
Hii mwafanya,
jamii itaja kasirika
Nchi mtakimbia.

Jonas John R

1 comment:

  1. Sikuwahi kufahamu kuwa wewe ni mkali wa mashairi. Hongera sana kijana.

    ReplyDelete