VYOMBO VYA HABARI NI KERO MGOMO WA WALIMU
Kila mtu na weledi wake. Taaluma ni kitu cha msingi sana. Kila mtu ni mjuzi katika fani aliyoisomea. Na leo hii ndio maana kuna mgawanyo wa kazi. Sio kila mtu afanye kazi zote.
Mwalimu akafundishe, mwana habari akatupashe habari, wanasiasa wakatudanganye, nakadhalika, nakadhalika.
Sote tunajua ambavyo walimu wamekuwa katika mgogoro wa kimaslahi na serikali uliowapelekea kugoma hivi juzi. Walimu hawa watakuwa halari kugoma iwapo wametimiza matakwa ya mgomo harali kama yalivyoainishwa katika sheria ya kazi na mahusiano kazini ya mwaka 2004, no 6 katika kifungu cha 80(1) (a)-(e).
Sheria hii pia katika kifungu cha 86(7)(a) kinataja wazi uhuru wa wafanyakazi kugoma iwapo CMA wameshindwa kutatua mgogoro wao wa kimaslahi.
Katika sheria hii hamna sehemu ilikoruhusiwa mgogoro wa kimaslahi kuupeleka mahakamani au kwa mtatuzi yaani Arbitrator. Kitendo cha Serikali kuamua kuupeleka mgomo wa wlimu mahakamani ni udhaifu na ni kudhiirisha kushindwa kwa serikali na kutapatapa.
Sasa kinachonitia wazimu hadi kichefuchefu ni hawa waandishi wa habari wasiojua chochote kuhusu migogoro na sheria mahala pa kazi kujitia kimbelembele kukosoa juhudi za walimu kudai haki zao.
Waandishi wa habari na watangazaji sijui kama wanaijua vema sheria ya kazi! Utasikia wakisema walimu wamo katika mgomo usio halari! Nani kasema si halari? Je, uhalari wa mgomo unategemea sheria au jinsi wewe unavyowaza!
Hacheni ushabiki na ukibaraka wa mambo msiyoyajua. Mahakama pekee ndiyo itasema iwapo mgomo ulikuwa harali au la lakini sio wewe uliyelala ukaamuka na mawazo yako ukatutangazia.
Kufanya kazi katika mazingira magumu, ujira mdogo, sheria ngumu za kazi na ubabe katika mazingira ya kazi havina budi kupingwa kwa nguvu zote n a kila mtanzania mwenye kutaka maendeleo.
Heko walimu, umoja, nguvu, pamoja.
No comments:
Post a Comment